Sunday, October 27, 2024

zilizopitaWakenya wataka mwanaharakati Boniface Mwangi kuachiliwa huru

 


Baadhi ya Wakenya wamepaza sauti wakitaka mwanaharakati Boniface Mwangi kuachiliwa huru baada ya kutekwa nyara nyumbani kwake alfajiri ya Jumapili na watu wasiojulikana.

Mke wake Njeri Mwangi amethibitisha tukio hilo kwenye akaunti yake ya mtandao wa X.

Kulingana na Njeri, Boniface alichukuliwa nyumbani na watu wasiojulikana mwendo wa saa moja asubuhi Jumapili.

Taarifa hizo zimezua hasira miongoni mwa Wakenya ambao wameilaumu serikali kwa kuhusika kwenye visa vingi vya utekaji nyara vinavyoshuhudiwa nchini Kenya.

Katika taarifa inayotazamiwa kuwa inaangazia kutekwa kwa Mwangi, aliyekuwa Rais wa chama cha mawakili nchini Kenya Eric Theuri ametaja hali ya polisi kuweka raia katika hali ya kuogopa na kuwazuia kutotoa maoni yao hadharani.

“Mapinduzi hubuniwa hivi. Matumizi ya njia zilizokuwa za kikatiba itachangia tu hali ya utawala huria.

“Visa vya watu kutekwa na matumizi ya polisi kukandamiza haki za watu kuwa na maoni kinzani na serikali kutaleta ukaidi zaidi. Siku moja, uoga utawatoka raia,’ Theuri alisema.

Mwandishi wa CNN Larry Madowo amezungumzia suala hilo kwa kusema kwamba visa vya utekaji nyara vimeendelea kuwanasa na kuwakandamiza wanaharakati na wapinzani wakuu wa serikali japo serikali imekanusha kuhusika.

“Mwanaharakati kutoka Kenya ametekwa nyara na watu wasiojulikana.#FreeBonifaceMwangi,” Alisema Larry Madowo kwenye Mtandao wa X.

Mwandishi mpekuzi John Allan Namu pia amezungumzia suala la ubakaji kwenye mtandao wa X : “ Hili linapaswa kukoma. #FreeBonifaceMwangi”.

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamelaani kutekwa kwa Mwangi.

Social centres working group wameshutumu kitendo hicho pia na kusema:

“Tunalaani vikali kitendo hicho kilichotekelezwa na maafisa wa serikali. Mwangi ni mwanaharakati wa haki za kibinadamu ambaye hajakosa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, alikuwa amepanga kuhudhuria mbio za Standard Chartered Marathon. Kuzuiliwa kwa Mwangi kinyume na sheria ni jambo la kuhuzunisha na kukiuka uhuru wa kujieleza. #FreeBonifaceMwangi

Kundi la The Defenders Coalition kwa upande wake limetaja hatua hiyo ya Mwangi kutekwa kama ukiukaji mkubwa wa haki zake za kibinadamu wakiongezea kwamba uchokozi wa aina hiyo hautakubalika.

Hata hiyo, polisi imetoa taarifa na kusema wanamzuilia katika kituo cha polisi cha Kamukunji jijini Nairobi

No comments:

Post a Comment

DRC: Kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila yapinga mradi wa kufanyia Katiba marekebisho

  Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyow...