Sunday, October 27, 2024

Mashambulizi ya Israel hayapaswi kupuuzwa, asema kiongozi mkuu wa Iran

 


Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei amesema kwamba mashambulizi ya anga ya Israel ambayo yalilenga Tehran na maeneo mengine siku ya Ijumaa usiku hayapaswi kupuuzwa wala kuonekana kuwa makubwa kuliko yalivyotokea.

Jeshi la Iran limesema kwamba wanajeshi wanne waliuawa kwenye shambulizi la anga ambalo jeshi la Israel lilisema lililenga maeneo ya kijeshi.

Khamenei amesema kwamba Israel ilifanya makosa ya kimkakati kuhusu Iran, jambo ambalo Tahran ni sharti ilifanyie kazi, kulingana na afisa aliyenukulina na kituo cha Habari cha kitaifa cha IRNA.

“Hawaifahamu vizuri Iran, “na” hawajaelewa kwa undani na vyema nguvu, uwezo na juhudi na ari ya taifa la Iran. Ni lazima tuelewe vizuri,” aliongezea.

Wanane wauawa kwenye shambulizi la Israel, yasema wizara ya afya ya Lebanon


Moshi unafuka angani baada ya shambulizi la Israel huko Sidon.

No comments:

Post a Comment

DRC: Kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila yapinga mradi wa kufanyia Katiba marekebisho

  Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyow...