Monday, October 28, 2024

DRC: Kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila yapinga mradi wa kufanyia Katiba marekebisho

 Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyowasilishwa na Rais Félix Tshisekedi wiki iliyopita. 


Rais wa Kongo Félix Tshisekedi (kushoto) na mtangulizi wake Joseph Kabila (kulia) walikuwa washirika mwanzoni mwa muhula wa rais Tshisekedi. Hapa, ilikuwa Januari 24, 2019

Na: Mercy Danson  DRC



Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni ya Jumapili Oktoba 27, muungano wa rais wa zamani umetoa wito wa "kuzuia" mageuzi kupitia "uhamasishaji". Kambi ya Joseph Kabila pia ilitaka kufanyia marekebisho katiba mwaka 2015, na kuamua kusitisha mradi huo baada ya kupingwa na maandamlano raia na Kanisa.

Nchini DRC, muungano wa Common Front for Congo (FCC) unapinga  mradi wa marekebisho ya Katiba na kutoa "wito wa kuhamasisha raia wa Kongo" ili kuzuia mradi huo. Watu "watasimama" "kutetea haki zao", "uhuru wao", muungano wa FCC unasema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumapili jioni.

Wiki iliyopita, akiwa Kisangani, Rais Félix Tshisekedi alithibitisha nia yake ya mageuzi hayo na akataja kuanzishwa mwaka 2025 kwa tume maalum ya wataalam.

No comments:

Post a Comment

DRC: Kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila yapinga mradi wa kufanyia Katiba marekebisho

  Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyow...